Image
Image

Wafuasi mashuhuri 20 wa kikundi Boko Haram wakamatwa*Buhari aapa kula nao sahani moja.

Majeshi ya usalama ya Nigeria yamewakamata wafuasi mashuhuri 20 wa kikundi cha wapiganaji cha Boko Haram kinachoshutumiwa kwa kuendesha mashambulio ya maafa nchini humo.
Rais MUHAMMADU BUHARI wa Nigeria ametangaza kipaumbele chake cha kupambana na kikundi hicho kilichoanza mapambano ya kutaka maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo yawe himaya ya Kiislam.
Takwimu zinaonyesha kuwa tangu Bwana BUHARI ashike madaraka tarehe 29 Mei mwaka huu wapiganaji hao wameuawa zaidi ya watu 700 katika mashambulio tofauti hasa maeneo ya Kaskazini-Mashariki mwa nchi hiyo.
Shambulio la hivi karibuni lilitokea kwenye kijiji kimoja kilichoko jimbo la Borno Kaskazini-Mashariki mwa nchi hiyo Ijumaa iliyopita ambapo watu 56 wamekufa.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment