Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,limekutana kuhusu amani na
usalama barani Afrika, likimulika hasa jitihada za kimataifa dhidi ya
mlipuko wa homa ya kirusi cha Ebola mwaka 2013.
Baraza hilo limehutubiwa kwa njia ya video na Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Afya Duniani, Margaret Chan akiwa Hong Kong, na Mjumbe Maalum
wa Katibu Mkuu kuhusu Ebola, Dkt. David Nabarro, akiwa Geneva.
Katika hotuba yake, Dkt. Margaret Chan amesisitiza umuhimu wa hatua
zimepigwa katika kukabiliana na Ebola, Guinea na Sierra Leone zikiwa
zimeripoti visa vitatu tu katika wiki mbili zilizopita, lakini akaonya
"Wakati huo huo, ni lazima nionye kuhusu kulegeza umakini. Inachukua
kisa kimoja kisichogundulika katika kituo cha afya, mtu mmoja
aliyeambukizwa kutoroka kutoka mfumo wa ufuatiliaji, au kisa kimoja cha
mazishi yasiyo salama kuibua tena visa vingi vya Ebola."
Naye Dkt. Nabarro amesisitiza umuhimu wa kuhusisha jamii katika jitihada za kukabiliana na mlipuko
"Hofu ya watu inakabiliwa kwa urahisi, tamaduni muhimu zinafanywa
kuwa salama na kuheshimiwa, mitandao ya maambukizi inagundulika haraka,
waliokaribiana na wagonjwa wanatambuliwa haraka na mlipuko unamalizika
haraka zaidi, iwapo jamii zinahusishwa katika jitihada."
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment