Hali ya hatari imetangazwa katika mji wa Ferguson, Jimbo la Missouri nchini Marekani kufuatia kijana mwingine mweusi kupigwa risasi na polisi mzungu na kujeruhiwa vibaya.
Kijana huyo TYRONE HARRIS mwenye umri wa miaka 18 alipigwa risasi wakati anashiriki kwenye maandamano ya maadhimisho ya mwaka mmoja ya mauaji ya kijana mwingine mweusi.
MICHAEL BROWN pia alipigwa risasi na kuuawa na polisi mzungu tukio lililozusha maandamano kote Marekani kupinga ubaguzi wa polisi kwa watu weusi na kulaumiwa pia kwa kutumia nguvu kupita kiasi.
Katika maadhimisho ya jana ya mauaji ya kijana MICHAEL BROWN polisi walikamata waandamanaji kadhaa waliozuia njia ya barabara.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment