Image
Image

Halmashauri kuu CCM yakamilisha kazi uteuzi wabunge*ACT wasema mgombea urais wake yupo*CHAUMA yaitaka NEC kukemea urasimu unaofanywa na watendaji.


Kamati kuu ya halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi imekamilisha kazi ya uteuzi wa wagombea ubunge katika majimbo mawili ya singida mashariki na kiteto huku ikiteua kamati ya kampeni yenye watu 32 kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao.

Kamati hiyo inaongozwa na katibu mkuu wa chama hicho Bw. Abdulrahiman Kinana ambapo walioteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika majimbo hayo mawili ni Bw.Jonathan Njau jimbo la Singida mashariki na Bw.Emmanuel John jimbo la kiteto majimbo ambayo yamechukuwa muda mrefu kujadiliwa na kutolewa maamuzi kwa lengo la kupata wagombea sahihi na wanaokubalika.

Akizungumzia suala la uvumi uliozushwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa ameenguliwa kwenye nafasi hiyo ya ukatibu uenezi na kukabidhiwa Mh.John Chiligati Bw.Nape mbali na kulaani uzushi huo amesema wakati huu ndiyo umuhimu wa sheria ya mitandaoni inaonekana kwani ingekuwa imeanza kazi kero kama hizo zisingekuwepo.

Wakati huo huo chama cha ACT wazalendo kimesema msimamo wake wa kupata mgombea urais bora uko palepale licha ya aliyeteuliwa na chama hicho Dk.Kitilia Mkumbo kuukataa uteuzi huo na kuongeza kuwa wana mtandao nchi nzima hivyo watahakikisha wanatumia muda mfupi uliobaki kupata wadhamini.


Katika tukio lingine mgombea urais kupitia tiketi ya chama cha CHAUMA Bw.Hashim Rungwe ameitaka tume ta taifa ya uchaguzi kuingilia kati kukemea urasimu unaofanywa na watendaji wa halmashauri katika zoezi la kuwasainia fomu za kugombea urais vinginevyo baadhi ya wagombea watashindwa kutimiza matakwa hayo ya kisheria.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment