Image
Image

Jeshi la polisi kitengo cha usalama Barabarani limeweza kudhibiti Asilimia 40% ya ajali zinazotokea.


Asilimia 40% ya ajali za Barabarani zinazotokea kwa sababu ya makosa hatarishi zimedhibitiwa kufuatia wadau wa mbali mbali ikiweo ITV/Radio one na Capital Radio,kuanzisha kampeni ya kuzuia ajali Barabarani.
Afisa mnadhimu wa makosa ya usalama barabarani nchini kamishna Johansen Kahatano amesema jijini Tanga katika mahojiano na ITV kuwa jitihada hizo zimesababisha katika kipindi cha miaka iwili iliyopita ajali za makosa hataraishi ikiwemo mwendo kasi ziepungua kwa asilimia 40% hatua ambayo imeonesha kuwa inaweza kuleta mafanikio na kupunguza vifo vya watanzania vitokanavyo na ajali.

Naye mkurugenzi wa ITV /RADIO ONE Bwana Deogratius Rweyunga amesema amewashukuru wadau wanaoshiriki katika kampeni hiyo na amewataka kuendelea kutoa ushirikiano wa kupiga simu zinazotangazwa kila siku kupitia mtandao wa Vodavom ambao utasaidia kuzidi kuleta mafanikio.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment