Baada ya minong”ono mingi ambayo
imekuwa ikiendelea katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii bila ya kuwa
na majibu ya kina kufuatia baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na
maendeleo chadema akiwemo Dkt.Wilbroad Slaa kutoonekana ndani ya chama hicho
baada ya kuingia Mh.Edward Lowassa kujiunga nao na kuwa mwanachama mpya ndani
ya CHADEMA hatimaye majibu yamepatikanana….
Moja ya viongozi ambao walikuwa
adimu kuonekana ndani ya Chadema ni katibu mkuu wa chama hicho,Dk.Willibrod, Naibu
katibu mkuu wa Chama,John Mnyika sambamba na Mwanasheria mkuu wa chama hicho Mh.Tundu
lissu,Ambapo kwa siku chache hizi John Mnyika, Tundu lissu wameonekana na
kushiriki katika vikao mbali mbali vya chama lakini wingu zito likabaki
kutawala vichwani mwa watu wengi wakijiuliza kuwa Dkt.Wilbroad Slaa kwamba
kutoonekana kwake kunaashiria nini ama penginene nikile kinachotajwa kuwa
huenda alikasirishwa na Ujio wa Mh.Lowassa angali nayeye alikuwa ana nia ya
kupeperusha bendera ya Chama hicho katika mbio za Urais,jambo lililoonekana
kama kapokonywa tonge mdomoni.
Majibu ya kwamba Slaa yupo wapi
na kwanini haonekani? Yameweza kupatiwa majibu ndani ya Baraza kuu la Chama cha
demokrasia na maendeleo Chadema kuwa Dkt.Slaa amepumzika siasa hivyo limeridhia
kwa maamuzi yake na hivyo litalazimika kusimamia kwa muda kazi za chama
alizokuwa akizifanya.
Katika ufunguzi wa mkutano wa
baraza kuu la chadema Mwenyekiti wa chama hicho taifa Freeman Mbowe amekiri
kuwa licha ya Dkt .Slaa kushiriki vikao mbalimbali vya chama kuhusu ujio wa Lowassa,lakini
ni kweli alitofautian kimtizamo na wajumbe wa kamati kuu.
Mh.Mbowe amekiri juu ya hofu iliyokwisha kutanda kwa viongozi,wanachama
na wapenzi wa chama hicho juu ya ujio wa baadhi ya vigogo kutoka ndani ya chama
cha mapinduzi CCM.
Kwa upande wake kaimu katibu mkuu
wa chadema taifa Salum Mwalimu akizungumza katika mkutano huo pamoja na masuala
mengine amewataka wanachama na wapenzi wa chama hicho kuahkikisha wanaunganisha
nguvu hasa katika kipindi cha uchaguzi
Miongoni mwa agenda kuu zilizojadiliwa katika baraza
kuu la chadema ni pamoja na agenda ya kupitisha ilani ya chama hicho,kupendekeza
majina ya wagombea nafasi ya urais ikiwa ni pamoja na kuthibitisha mikakati na
rasilimali za kuendesha kampeni za uchaguzi mkuu.
Ni kishindo cha baraka za baraza
kuu la chadema likiridhia kupumzika kwa Dk.Wilibroad Slaa ambaye tangu kujiunga
kwa waziri mkuu Mstaafu Edward Lowasa amekuwa haonekani katika vikao nyeti vya chama hicho.
Wachambuzi wa mambo na wadau
mbali mbali wamekuwa na mijadala ya kimya kimya kutafakari uamuzi aliouchukua Dkt.Slaa
kwamba kweli nimaamuzi kutoka moyoni ama nikama ambavyo inatajwa kuwa amepokonywa
tonge mdomoni?.Wanasema kama ni maamuzi yakwakwe mwenyewe inakuwaje chama hicho
katika kipindi hiki kinacho hitaji ushindi akashindwa kusubiri mchakato
ukamilike hadi kupata ushindi na kuchukua dola ndipo aweke maamuzi yake,kama
haitoshi wakaangalia mbali zaidi kulikuwa na Ugumu gani kujitokeza wakati
Mh.Lowassa ambaye kachukua Fomu ya kuwania urais ndani ya chama hicho kumpa
ushirikiano ili ushindi uje nyumbani?.
Miongoni mwa moja ya maswali yayayo
kanganya watanzania wengi ni hayo ambayo mwisho wa siku wanaamini huenda
wakapata majibu mazuri zaidi juu ya hatima yake isije ikawa ameweka wazi
kustaafu siasa mwisho wasiku tukamsikia yupo chama Fulani kama ilivyokuwa
ikitajwa kwamba anamchakato wa kukihama chama hicho cha Demokrasia na maendeleo
CHADEMA,Wapi atakapo enda anapo tataji,bado hayajawa wazi ila kama atakuwa na
mchakato huo ataweka wazi.
0 comments:
Post a Comment