RAIS Jakaya Kikwete anatarajiwa kuzindua rasmi benki ya kwanza ya
Maendeleo ya Kilimo nchini kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa
Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam kesho.
Akizungumza jana, Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo, Thomas Samkyi,
alisema dhumuni kuu la uanzishaji wa benki hiyo ni kuboresha tija katika
uzalishaji kwenye sekta ya kilimo kwa kuunganisha nguvu za wadau
mbalimbal.
Alisema benki hiyo itaendeleza miundombinu ya kilimo kama miradi ya
umwagiaji, usafirishaji, uhifadhi na mindombinu ya masoko, ambayo
inachangia maendeleo ya sekta ya kilimo. Aliongeza kuwa benki hiyo
inalenga kuziba mianya mikubwa ya ukopeshaji kwenye kilimo, ambayo
inaachwa na benki za biashara.
Aidha, alisema benki hiyo itachochea kukua kwa sekta ya kilimo kwa
kutoa mikopo wakulima, ambao wengi wao hawana uwezo wa kupata huduma za
kibenki. “Benki hii imeundwa ili kutoa mikopo kwa masharti nafuu na
kutoa huduma nyinginezo zitakazoongeza uwezo wa wakulima kukopa na
kuzalisha na ili kufanikisha hilo benki inabidi iwe na vyanzo endelevu
vya fedha za kutosha kwani nchi hii ni kubwa na wadau wa benki ni
wengi,” aliongeza Samkyi.
Aliongeza kuwa itakuwa ikifanya kazi kwa ukaribu zaidi na benki
washirika, ambao watafanya nao kazi katika kuwakopesha wakulima hao.
Alisema watafungua ofisi kwa kanda na kutakuwa na utaratibu maalumu wa
urejeshaji wa mikopo, ambapo sio kila mwezi, bali itakuwa ni kila msimu
wa mavuno.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment