Image
Image

Lishe bora kwa watoto:Jinsi ambavyo kuondoa vikwazo kwa unyonyeshaji,kutaokoa maisha ya watoto.

Ripoti hii iliyochapishwa na shirika la Save the Children, inatoa wito ili umuhimu wa kunyonyesha watoto wachanga utambuliwe na hivyo msaada utolewe ili kufanikisha hilo. Likitumia ushahidi wa hivi karibuni, shirika hilo linafafanua ni jinsi gani unyonyeshaji watoto wachanga unaokoa maisha na kutoa kielelezo cha hali ya unyonyeshaji watoto duniani kote.
Ripoti hiyo inachambua sababu za kutokuwepo maendeleo kwenye viwango vya unyonyeshaji na kuorodhesha vikwazo vinne vinavyowazuia akinamama kunyonyesha watoto wao:
1)     Vikwazo vya kitamaduni na kijamii
2)     Upungufu wa wahudumu wa afya
3)     Kutokuwepo sheria zinazosisitiza masuala ya uzazi
4)     Uuzaji wa vyakula mbadala usiodhibitiwa
 Ripoti hiyo imehitimishwa kwa kutoa mapendekezo  ya jinsi ya kuongeza kiwango cha unyonyeshaji:
1) Kupinga desturi za kiutamaduni na kijamii zinazokinzana na umuhimu wa unyonyeshaji
2) Kuiboresha mifumo ya afya ili ilinde, ihamasishe na kuchochea unyonyeshaji
3) Kuweka sera na sheria zinazohusu unyonyeshaji na kusimamia utekelezaji wake nchi nzima.
4) Kuimarisha usimamizi wa utendaji wa sekta ya vyakula mbadala.
Taarifa na ujumbe muhimu:
  • Mnamo 2011, watoto milioni 6.9 walio chini ya miaka mitano walifariki.
  • Tangu 1990, idadi ya watoto waliofariki kwa mwaka ilipungua kwa watoto milioni 5. Idadi hiyo ni pungufu ya watoto 14,000 wanaokufa kila mwaka.
  • Inakadiriwa vifo 830,000 vya watoto wachanga vinaweza kuepukika kama kila mtoto angenyonyeshwa ndani ya saa moja tangu kuzaliwa.
  • Katika yale masaa ya mwanzo na pia siku za mwanzo baada ya kujifungua, mwili wa mama hutengeneza maziwa ya awali yanayoitwa colostrum. Maziwa haya thamani yake ya ubora katika virutubisho vya ulinzi wa afya kwa mtoto ni kubwa isiyo na mfano,
  • Inakadiriwa asilimia  22% ya vifo vya watoto wachanga vingeweza kuzuilika kama unyonyeshaji ungeanza ndani ya saa moja baada ya mtoto kuzaliwa, na asilimia 16% wangeokolewa kama unyonyeshaji ungeanza katika siku ya kwanza ya kuzaliwa.
  • Mtoto mchanga anayenyonyeshwa ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa uwezekano wake wa kuishi ni mara tatu zaidi ya yule anayeanza kunyonyeshwa siku moja baadae.
  • Katika miezi sita ya mwanzo baada ya kuzaliwa, watoto ambao hawajanyonyeshwa wana hatari ya kufariki kwa homa ya mapafu mara 15 zaidi, na mara 11 zaidi wanaweza kufariki kwa kuhara, ukilinganisha na wale ambao wemenyonyeshwa ziwa la mama peke yake (angalia taarifa zaidi kwenyekipeperushi).
  • Duniani kote, katika kila watoto watatu, wawili kati yao wanalishwa vyakula vyenye ubora hafifu, au mchanganyiko wa maziwa ya mama na vyakula vingine.
  • Biashara ya maziwa ya kwenye mikebe inakadiriwa kuwa nathamani ya Dola za Kimarekani bilioni $25 (takriban 40 trilioni/-).
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment