TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeanza mazoezi katika Uwanja
wa Karume kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria kuwania kufuzu kwa
Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2017 nchini Gabon.
Wachezaji wa Taifa Stars chini ya kocha wake mkuu Charles Mkwasa
watakuwa wakijifua mara mbili kwa katika Uwanja wa Karume katika
kujiweka sawa na maandalizi ya mchezo huo.
Kufuatia baadhi ya wachezaji kuwa na majukumu na timu zao kujiandaa
na mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa Agosti 22, Mkwasa amewaongeza
wachezaji wengine kumi (10) kutoka katika orodha yake ya akiba.
Lengo la kambi hii ya awali ya siku tano, ni kupata nafasi ya kuwaona
wachezaji katika mazoezi hayo kabla ya safari ya kuelekea nchini
Uturuki Agosti 23 mwaka huu kwa kambi ya siku kumi.
Wachezaji walioitwa na kuanza mazoezi ni Said Mohamed, Vicent Andrew
(Mtibwa Sugar), Mohamed Hussein, Ibrajim Ajibu (Simba SC), Hamis Ali,
Juma Mbwana (KMKM), Tumba Sued (Coastal Unioni), Samuel Kamuntu (JKT
Ruvu), Ibrahim Hilka (Zimamoto– Zanzibar) na Mohamed Yusuf (Prisons).
Wachezaji wengine waliopo kambini ni Said Ndemla, Hassan Isihaka,
Abdi Banda(Simba SC), Rashid Mandawa (Mwadui FC), Michael Aidan (Ruvu
Shooting), Orgeness Mollel (Aspire Academy) na Abdulhaman Mbambi
(Mafunzo).
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment