Rais Erdogan afahamisha kuwa Uturuki itapambana na ugaidi hadi pale hakutokuwa na gaidi hata mmoja katika ardhi ya Uturuki.
Rais Recep Tayyip Erdogan amefahamisha kuwa mapambano dhidi ya ugaidi yataendela hadipale hakutopatikana gaidi hata mmoja nchini Uturuki.
Rais Erdogan aliyafahamisha hayo katika hafla ya kutoa taji kwa mkuu wa majeshi Necdet Ozel ambae muda wake wa kuhudumia taifa umefikia kikomo
Rais Erdogan alizidi kufahamisha kuwa mashambulizi dhidi ya ugaidi yataendelea hadipale magaidi watakaposalim amri na kuweka silaha chini na kusitisha mashambulizi dhidi ya raia na kutaka kuharibu taifa.
Alimalizia akifahamisha kuwa sote tunafahamu uharibifu unaosababishwa na ugaidi pande zote za dunia, ni wajibu wetu kupambana.
0 comments:
Post a Comment