Halmashauri
ya Manispaa ya Iringa imeanza kupunguza maambukizi ya virusi nya ukimwi na
magonjwa mengine ya zinaa baada ya vijana kuanza kuhudhuria kliniki ya huduma
rafiki kwa vijana zihusuzo afya ya uzazi na mtoto zinazotolewa katika zahanati
mbalimbali za manispaa ya iringa zinazohusisha matibabu pamoja na elimu ya
namna ya kujikinga na magonjwa hayo
Mganga mkuu wa halmashauri ya
manispaa ya iringa dokta mei alexander amesema hayo wakati alipopokea vifaa
mbalimbali katika zahanati tano vilivyotolewa na shirika lisilo la kiserikali
la amref chini ya mradi wa (afya ya uzazi ni haki ya kijana tuitetee) ambapo
mradi huo umekamilisha utoaji wa vifaa tiba pamoja na ukarabati wa majengo ya
zahanati tano za manispaa hiyo ili ziendane na huduma rafiki zinazoweza
kuwavutia vijana.
Akizungumza
na itv kwenye zahanati ya kitwiru muuguzi mkuu wa zahanati hiyo esther sanga
amesema wamefanikiwa kuongeza idadi ya vijana wanaohudhuria kliniki baada ya
kuhamasisha vijana kwa kutumia mikutano ya hadhara hiyo ikiwa ni baada ya
wahudumu wenyewe kupatiwa mafunzo yaliyofadhiriwa na shirika hilo la amref hali
ambayo imesaidia siyo tu kupunguza maambukizi ya magonjwa zinaa bali pia mimba
za utotoni.
Kwa upande
wake meneja miradi ya afya uzazi mama na mtoto amref benatus sambili amesema
shirika hilo liliamua kupeleka mradi huo wa miaka mitano wenye thamani ya dola
milioni 600 za kimarekani uliotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano katika
halmashari za manispaa ya iringa,ilala na kinondoni baada ya kuona mahitaji ya
maeneo husika na kwamba mradi umesaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza idadi ya
vijana wanaopata huduma za afya ya uzazi.
0 comments:
Post a Comment