Kuongezeka kwa matumizi ya makaa, petrol na gesi asili kila uchao kumepelekea kuongezeka kwa kasi ya kubadilika kwa hali ya hewa, kupotea kwa misitu na kuharibika kwa mazingira.
Kiwango cha Kaboni dioksidi kimeongezeka kutoka chembe 280 kwa milioni hadi chemebe 394 kwa milioni. Kiwango hicho kinafaa kudumishwa chini ya chembe 350. Kuongezeka kwa kiwango cha kaboni dioksidi katika hewa kunapelekea kuongezeka kwa kiwango cha joto kwa nyuzi 1.
Ingawa nyuzi moja inaonekana kuwa ndogo athari yake katika ustawi wa mazingira ni kubwa mno.
Kiwango hichi cha joto husababisha mawimbi ya joto yanayopuliza , mvua inayopita kiasi na hali nyingine ya hewa ambayo imepita kiasi.
Jopo la kimataifa kuhusiana na mabadiliko ya hali ya anga lilikubaliana kuwa ili kupunguza kiwango cha joto kwa nyuzi mbili ni lazima kuwa na njia ya kudhibiti kiwango cha gesi kama vile kaboni dioksidi inayoongeza kiwango cha joto kwenye hewa. Jopo hilo lilisema kuwa iwapo mwenendo wa kuongezeka kwa gesi hewani utaendelea basi hali ya hewa itaweza kufikia viwango ambavyo hatutaweza kurekebisha.
Hali kama vile viwango vya juu vya joto, mafuriko ya mara kwa mara yatakuwa mambo ya kawaida.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na wanasayansi kiwango cha gesi za joto kama vile kaboni dioksidi katika hewa kinafaa kupunguzwa kwa asilimia 25 kufikia mwaka wa 2020 na kwa asilimia 80 kufikia mwaka wa 2050.
Ingawa nchi kadhaa zimchukua hatua katika kufikia lengo hili bado hakuna hatua ya pamoja iliyoafikia na mashirika ya kimataifa a una nchi za kimataifa.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka kwa taasisi ya takwimu ya Uturuki kiwango cha gesi kimeongezeka kwa asilimia 124 ikilinganishwa na mwaka wa 1990.
Zifuatazo ni baadhi ya hatua zinazoweza kuchukuliwa kupunguza kiwango cha gesi za joto angani
- Kutumia zaidi usafiri wa umma
- Kuhakikisha kuwa barabara zetu zipo salama kwa ajili ya matumizi ya baiskeli na kwa wanaotembea kwa miguu
- Kutumia zaidi vyanzo vya nishati kama vile Jua na upepo.
- Kurejelezwa kwa taka inayoweza kurejelezwa.
Kwa wakati wa sasa nchi tofauti zinajaribu kuanzisha miradi mbalimbali ya kulinda mazingira na kuhakikisha kuwa hali ya hewa haiharibiwi.
Hata hivyo hatua zilizopigwa bado hazitoshi.
Ni lazima hatua zaidi zichukuliwe ili kuokoa maisha sio tu ya baadae bali pia ya sasa.
0 comments:
Post a Comment