Snoop Dogg akamatwa akiwa na kitita cha pesa 400,000 sarafu za Marekani nchini Italia.
Msani wa muziki kutoka Marekani katika jimbo la California amekamatwa Jumamosi katika uwanja wa ndege wa Lamezia na Polisi ya Italia akiwa na kitita cha pesa 400,000 sarafu za Marekani katika mto.
Tukio hilo limetokea Julai 1 katika uwanja wa ndege wa Lamezia Terme kusini mwa Italia.
Snoop Dogg ambae jina lake halisi ni Calvin Broadus alikuwa katika matamasha mawili kusini mwa Italia ambapo alikuwa akitaraji kujielekeza nchini Uingereza kushiriki katika tamasha la Kendal Calling nchini humo.
Serikali ya Italia inapiga marufuku mtu kuwa na pesa taslim zaidi ya 10,000.
Mawakili wanne wa Snoop Dogg wamefahamisha kufuatilia kesi hiyo ili pesa hizo zirejeshwe hata kama itakuwa baada ya kutolewa wa faini.
Juma lililopita msanii huyo wa hip-hop alikamatwa nchini Uswidi baada ya kuonekana katika hali ya ulevi na kauchiwa huru muda mchache baada ya kufanyiwa uchunguzi.
0 comments:
Post a Comment