MABASI maalumu kwa ajili ya kutoa huduma chini ya mradi wa mabasi yaendayo haraka yameingia nchini tayari kwa kuanza huduma.
Kampuni ya ubia ya UDART kwa kushirikiana na wakala wa mabasi
yaendayo haraka (DART) inaanza leo kuendesha mafunzo kwa madereva kabla
ya huduma ya usafiri kuanza rasmi Oktoba. Mabasi mawili yaliyoingizwa
nchini ndiyo yatatumiwa katika mafunzo hayo.
Jana mabasi hayo yenye uwezo wa kubeba abiria wapatao 190 na jingine
la abiria 100, yalipitishwa kwenye njia yake kuanzia Kivukoni hadi
Ubungo na umma kutambulishwa juu ya mafunzo hayo leo.
“Kesho (leo) tunazindua mabasi mawili kwa mafunzo. Wakufunzi wametoka
China...huduma kamili inaanza Oktoba,” Alisema Meneja wa Udart, Sabri
Mabruk katika mkutano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari. Ujio
wa mabasi hayo na kuanza kwa huduma za BRT, kwa mujibu wa Mabruk, ndiyo
mwisho wa daladala za kawaida kati ya Kimara na Kivukoni.
Alisema kutakuwa na utaratibu wa kulipa gharama za usumbufu kwa wenye mabasi na kisha kuwapangia njia nyingine.
Idadi ya mabasi yanayotarajiwa kutoa huduma chini ya mradi, ni 76.
Mabruk alisema mwezi ujao ndio watajua ni mabasi mangapi mengine
yataletwa. Baada ya mafunzo ya wiki mbili kwa madereva, mabasi yaliyoko
yatatoa huduma kupitia vituo 10 pekee kabla ya Septemba ambayo idadi ya
mabasi itakuwa imekamilika.
Mabasi hayo yanayotarajiwa kutumia dakika 20 kutoka Kimara hadi
Kivukoni eneo la Magogoni, ndani yana viti kwa ajili ya wazee,
wajawazito na wenye ulemavu.
Pia yana mikanda maalumu ya kushika kwa abiria wanaosimama. Vile vile
ilielezwa hayatakuwa na makondakta wala wapiga debe kutokana na mfumo
wake wa kisasa wa ukusanyaji nauli.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment