Kishindo cha kura za maoni ndani ya CCM kimeendelea kuwakumba baadhi ya vigogo wa chama hicho baada ya jana mawaziri wengine watano kuanguka.
Miongoni mwao ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mathias Chikawe aliyekuwa akiwania kupitishwa tena kugombea tena
ubunge wa Nachingwea.
Chikawe ambaye pia alishindwa
katika kinyang’anyiro cha urais kupitia chama hicho, alidondoshwa na
Hassan Masala aliyepata kura 6,494 akifuatiwa naye akipata 5,128.
Wagombea
wengine ni Steven Nyoni (1,438), Amandus Chinguile (1,274), Fadhili
Liwaka (1,171), Benito Ng’itu (797), Greyson Francis (671), Albert Mnali
(763), Issa Mkalinga (466), Mustafa Malibiche (427) na Ali Namnjundu
(319).
Mbali ya Chikawe pia manaibu waziri wanne
wameangushwa katika kura hizo. Hao ni Mahadhi Juma Maalim (Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa), Perera Ame Silima (Mambo ya Ndani), Amos
Makala (Maji) na Saning’o ole Telele (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi).
Mahadhi
alianguka katika Jimbo la Paje, Zanzibar kwa kupata kura 1,785 huku
Jaffar Sanya Jussa ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) Mkoa wa
kusini akiibuka mshindi kwa kura 3,368.
Silima aliyepata kura 1,218 katika Jimbo la Chumbuni alibwagwa na mpinzani wake, Ussi Pondeza aliyepata kura 1,952.
Katika
Jimbo la Mvomero, Suleiman Murad alishinda kwa kura 13,165 dhidi ya
Makalla ambaye alikuwa anatetea jimbo hilo akipata 10,973.
Ole
Telele alipata kura 5, 126 huku William ole Nasha akiibuka mshindi kwa
kura 23, 563 akifuatiwa na Elias Ngolisa aliyepata 11, 442 na Dk
Eliamani Lalkaita 7,135. Matokeo hayo hayakujumlisha kura za matawi
matano ambayo Katibu wa CCM Wilaya ya Ngorongoro, Elihudi Shemauya
alisema hayawezi kubadili matokeo.
Katika Jimbo la
Uzini, Katibu wa Oganizesheni wa CCM, Muhammed Seif Khatib ameshindwa
baada ya kupata kura 1,333 huku mpinzani wake Salum Mwinyi Rehani
akiibuka kidedea kwa kura 1,521.
Kigogo mwingine wa
CCM, Nape Nnauye ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi, ameshinda kura
hizo Jimbo la Mtama kwa kura 9,344 dhidi ya mpinzani wake Selemani
Methew aliyepata kura 4,766.
Jimbo la Chwaka mbunge wa
jimbo hilo kwa miaka 20, Yahya Kassim Issa aliangushwa baada ya kupata
kura 1,572 dhidi ya mpinzani wake, Baguwanji Mensuriya Baguwanji
aliyepata kura 1,951.
Wakati mawaziri hao wakianguka,
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya alishinda katika jimbo jipya la Welezo huku
Waziri wa Ulinzi, Hussein Mwinyi akishinda katika Jimbo la Kwahani.
Aliyekuwa
Mwenyekiti wa UVCCM, Masauni Hamad Masauni ameshinda Jimbo la Kikwajuni
kwa kura 2,222 dhidi ya mpinzani wake, Mussa Shaali Choum aliyepata
kura 461.
Katika Jimbo la Jang’ombe, Ali Hassan Omar
ameibuka mshindi kwa kupata kura 879 dhidi ya mpinzani wake Abdullah
Hussein Kombo (639).
Aliyekuwa Waziri Kiongozi Zanzibar
na waziri wa zamani wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai
Nahodha aliibuka mshindi katika Jimbo la Kijito Upele.
Jimbo
la Malindi Abdullah Juma Abdulla alishinda kwa kura 558 dhidi ya
mpinzani wake, Kombo Mshenga Zubeir aliyepata kura 241. Jimbo hilo
nafasi ya uwakilishi, Mohammed Ahmada Salum alishinda kwa kura 336 na
dhidi ya Abdulrahman Hassan (271).
Majimbo mengine
Liwale: Faith Mitambo (7,238), Zainabu Kawawa (3,126).
Ruangwa: Naibu Waziri (Tamisemi), Kassim Majaliwa (11,988), Bakari Nampenya (2,678).
Kilwa Kaskazini: Murtaza Mangungu alishinda kwa kura 7,140.
Kilwa Kusini: Hasanain Dewji ameshinda kwa kura 3,859.
Lindi Mjini: Hassani Kunje (3,428) Mohamedi Ulthali (2,314).
Jimbo la Mchinga: Said Mtanda ameshinda kwa kura 3,101, Riziki Lulida (2,217).
Serengeti:
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Kebwe Steven Kebwe aliibuka
mshindi kwa kura 29,268 akiwashinda, Dk James Wanyancha (5,980) na
Mabenga Magonera (1,638).
Nyamagana: Aliyekuwa Meya wa
Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula ameibuka mshindi kwa kura 9,553, Joseph
Kahungwa (3,947) na Raphael Shilatu (894) na kufuatiwa na wenzao 17.
Ukerewe:
Christopher Nyandiga aliongoza kura 8,077, Gerald Robert (142), Laurent
Munyu (197), Emmericiana Mkubulo (242), Bandoma Kabulule (414), Bigambo
Mtamwega (477), Dk Elias Missana (648), Hezron Tungaraza (693), Dk
Deogratias Makalius (727), John Mkungu (775), Osward Mwizalubi (1,098),
Maliki Malupu (1,443), Deogratias Lyato (1,824), Sumbuko Chipanda
(2,016) na Magesa Boniphace (2,552).
Morogoro Mjini: Abdulaziz Abood amepata kura 20,094 na Simon Berege (429).
Mikumi: Jonas Nkya alipata kura 947 ameshinda dhidi ya Abdulsalum Sas (544).
Kilombero:
Mbunge wa jimbo hilo, Abdul Mteketa alianguka baada ya kushika nafasi
ya tatu kwa kupata kura 2,646 nyuma ya Abubakar Assenga aliyepata kura
6,629 na Abdul Liana 3,999.
Mlimba: Godwin Kunamba ameshinda kwa kura 6,233 Dk Fredrick Sagamiko (2,203), Jane Mihanji (2,073).
Gairo: Mbunge wa sasa, Ahmed Shabiby alishinda kwa kura 15,920 akifuatiwa na Omari Awadhi 886.
Morogoro
Kusini Mashariki: Omary Mgumba alishinda kwa kura 3,393 akifuatiwa na
Jamila Taji (2,914) na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Dk Lucy Nkya
(1,710).
Msoma Vijijini: Profesa Sospeter Muhongo
aliibuka mshindi kwa kura 30,431 waliofuatia ni Anthony Mtaka (3,457),
Evarest Mganga (2,556), Profesa Edson Mjungu (898), Mafuru Mafuru (421),
Wits Onyango (392) na Nelson Semba (186).
Butiama:
Nimrodi Mkono ameshinda kwa kupata kura 19,366, Chirstopher Siagi
(2,457), Samweli Ndengo (745), Jacob Thomas (502), Mwita Wariuba
(1,346), Moringe Magige (317), Godfrey Wandiba (303), Joseph Nyamboha
(262) na Samweli Gunza (73).
Musoma Mjini: Vedastus
Mathayo alishinda kwa kura 6,691 akifuatiwa na Paul Kirigini (1,174), Dk
Msuto Chirangi (1,082), Juma Mokili (681), Deus Mnasa (378), Nicodemus
Nyamajeje (183), Emmanuel Mwita (155), Felix Mboje (131) na Zerulia
Mneno (61).
Kyela: Waziri wa Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Dk Harrison Mwakyembe ameshinda kwa kupata kura 15,516,
George Mwakalinga (4,905) na Martin Kipija (2,301).
Njombe
Kusini: Edward Mwalongo (3,870), Romanus Mayemba (2,153), Daniel
Msemwa (1,976), Arnold Mtewele (1,136), Alfred Luvanda (978), Hassan
Mkwawa (152), Vitalis Konga (76) na Mariano Nyigu (86).
Makambako: Deo Sanga (7,643) Alimwimike Sahwi (499).
Ludewa:
Deo Filikunjombe kabla ya kata tatu alikuwa na kura18,290 akiwaacha
Kapteni Jacob Mpangala (205) na Zephania Chaula (770).
Wanging’ombe;
Gerson Lwenge kabla ya kata tatu alikuwa na kura 11,322, Thomas Nyimbo
(1,871), Yono Kevela (1,819), John Dugange (466), Richard Magenge
(417), Abraham Chaula (382), Kennedy Mpumilwa (332), Hoseana Lunogelo
(322), Malumbo Mangula (304), Nobchard Msigwa (216), Abel Badi (106) na
Eston Ngilangwa (47).
Kiteto: Mjumbe wa NEC, Emmanuel
Papian ameshinda kwa kupata kura 40,636 mbunge aliyemaliza muda wake
Benedict Ole Nangoro (21,461), Amina Said Mrisho (2,118), Ally Lugendo
(287) na Joseph Mwaseba (250).
Bunda Mjini: Waziri wa
Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira ameshinda kwa kupata kura
6,429 dhidi ya kura 6,206 alizopata mshindani wake wa karibu, Robert
Maboto. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Christopher Sanya alipata
kura1,140, Exavery Lugina (846), Simon Odunga (547), Magesa Mugeta
(446), Peres Magiri (385) na Brian Bitta (263).
Handeni na Bumbuli
Waziri
wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda pamoja na Naibu Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba wameshinda katika
mchakato wa kura za maoni katika majimbo ya Handeni na Bumbuli.
0 comments:
Post a Comment