Mbowe alisema hayo jana katika Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach kilipokuwa kinafanyika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema jana.
“Siwezi
kusema zaidi ya hapo,” alisema Mbowe alipoulizwa sababu za kutokuwapo
Dk Slaa katika vikao hivyo muhimu na kuongeza atatoa baadaye, mrejesho
wa kikao hicho.
Kauli hiyo ya Mbowe haikuondoa wingu
zito lililotanda Chadema baada ya kutoonekana hadharani kwa kiongozi
huyo katika matukio manne muhimu ya chama hicho kikuu cha upinzani,
tangu waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa ajiunge nacho.
Tofauti
na Dk Slaa, Naibu Katibu Mkuu (Bara), John Mnyika alionekana jana kwa
mara ya kwanza katika kikao hicho na kufuta uvumi uliokuwa umesambaa
kuwa alikuwa na mpango wa kuachana na Chadema kama inavyodaiwa kwa Dk
Slaa.
Viongozi hao walianza kutoonekana katika shughuli
za chama tangu Lowassa alipojiunga na Chadema Julai 28 na kukabidhiwa
fomu ya kugombea urais Julai 30 na juzi Agosti Mosi alipozirejesha.
Hata
hivyo, viongozi waandamizi wa Chadema wamesema suala la kutokuwapo kwa
Dk Slaa halipaswi kukuzwa kwa kuwa ‘anafanya kazi nyingine za chama.’
Alipoulizwa
jana, Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu alisema: “Suala la
kutokuwapo Dk Slaa ni kitu cha kawaida, anafanya kazi nyingine huko,
lakini pia kuna wasaidizi wake hapa ambao ni sisi manaibu. Mlikuwa
mnazungumzia Mnyika naye haonekani, si huyo. Hatuwezi kuendelea kujibu
‘rumors’ (uzushi) wa kwenye mitandao… nyie subirini si tupo mtaona kama
yupo au la.”
Mnyika atinga kikaoni
Jana, Mnyika alionekana katika viwanja vya hoteli hiyo lakini alikataa kuzungumzia kwa undani suala hizo.
“Siwezi
kuzungumza chochote,” alisema Mnyika na hata alipoulizwa ni lini
atawaeleza Watanzania juu ya kutoonekana kwake alisisitiza mara tatu
kuwa “Siwezi kuzungumza chochote.”
Chama hicho
kinaendelea na mfululizo wa vikao vya vyombo vya juu ambapo leo
kinatarajia kutafanya kikao cha Baraza Kuu kabla ya Mkutano Mkuu kesho
kumpitisha mgombea wa urais kesho.
Kura za maoni Kibamba zaahirishwa
Mchakato
wa kura za maoni wa kumpata mgombea wa ubunge wa chama hicho katika
Jimbo Kibamba utafanyika leo baada ya kuahirishwa juzi.
Kaimu
Katibu wa Chadema Mkoa wa kichama Kinondoni, Rose Mushi alisema kura
hizo zitapigwa leo kuanzia saa nne asubuhi, Kimara Baruti. “Kila kitu
kinakwenda vizuri, nadhani kesho (leo), tutafanya mchakato huu wa kura
za maoni, kama kutakuwa mabadiliko nitakutaarifu,” alisema Mushi.
Awali,
Mratibu wa Chadema Kanda Pwani, Casmir Mabina alisema: “Jana (juzi),
tulishindwa kufanya kwa sababu mmoja wa watia nia alikuwa mgonjwa.
Hakupata taarifa za mchakato huo, tukatumia demokrasia ya kuahirisha.”
Mwenyekiti
wa Jimbo la Ubungo, Boniface Jacob alisema kura za maoni katika jimbo
hilo (Kibamba) huenda zikafanyika leo baada ya kupokea taarifa kutoka
kanda. “Sisi kazi yetu ni kuratibu mchakato wa kura za maoni ila
maelekezo yote yanatoka juu, inawezekana ikiwa kesho (leo) jioni sina
uhakika,“ alisema Jacob.
Juzi, hali ya sintofahamu
iliwakumbuka wajumbe na watia nia wa jimbo hilo baada ya kufika kwenye
ukumbi wa mikutano na kuambiwa kuwa mchakato wa kura za maoni
umeahirishwa kwa madai kuwa mmoja ya watia nia hakupewa taarifa.
Hatua
hiyo ilizua minong’ono miongoni wa wajumbe na watia nia ambao waliokuwa
wamejiandaa kwa mchakato huo wakidai kuna hujuma zinataka kufanyika.
0 comments:
Post a Comment