Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya
Mungano na ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na mmoja ya kiongozi wa
juu wa CCM taifa ni miongoni mwa vigogo wa Chama cha Mapinduzi walioangushwa
katika kura za maoni za CCM
Zanzibar.
Upigaji wa kura hizo umefanyika
katika maeneo mbali mbali huku majimbo
mengine yamelazika kurudia baada ya
kutokea utata wa kadi na karatasi za kura ikiwemo jimbo la Mahonda amablo
Makamu wa Pili wa Rais, Balozi SEIF ALI IDDI
anawania Uwakilsihi pamoja na KIDAWA ALI
anawania Ubunge.
Kwa mujibu wa taarifa za Mkoa wa
Kusini Unguja,Naibu Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikano wa Kimatifa,MAHADHI MAALIM ameshindwa na mjumbe wa NEC IBRAHIM
SANYA.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,PEREIRA AME SILIMA
naye ameshindwana kijana wa jimbo la
Chumbini, kwa upande wa Zanzibar waziri
asiyekuwa Na Wizara Maalum SULEIMAN
NYANGA naye ameangushwa katika
Jimbo la Jang'ombe, huku Naibu Waziri wa
Biashara, THUYWA KISASI naye ameshindwa Jimbo la Fuoni.
Mbunge wa uzini kwa miaka zaidi ya 20 na Katibu wa Sekratriet ya CCM taifa ya
organaisheni, MOHAMED SEIF KHATIB naye
ameangushwa wakati Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, HUSSEIN MWINYI ametetea kiti chake cha
Kwahani.
0 comments:
Post a Comment