Image
Image

Mazungumzo ya amani ya kujaribu kupata muafaka kwa mahasimu wa kisiasa Sudani Kusini kufanyika Ethiopia.

Duru ya tatu ya mazungumzo ya amani ya Sudani ya Kusini inatarajia kuanza leo huko Addis
Ababa, Ethiopia kujaribu kupata muafaka wa kumaliza mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo.
Rais SALVA KIIR na kiongozi wa waasi Bwana RIEK MACHAR wanatarajia kuhudhuria mazungumzo
hayo yanayoendeshwa kwa upatanishi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Nchi za Afrika Mashariki
na Pembe ya Afrika IGAD.
Kwa mujibu wa IGAD mazungumzo hayo, chini ya msukumo mpya, yanatakiwa yamalizike
Jumatatu hiyo ambapo pande zote kabla ya kuondoka Ethiopia zitatakiwa kutia saini
makubaliano ya amani.
Lakini Bwana RIEK amesema haielekei kama makubaliano hayo yatafikiwa kutokana na kile
alichodai kubadilishwa kwa mapendekezo ya awali ya makubaliano.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment