Na Upendo Mosha, Mwanga
RAISI Jakaya Kikwete jana aliongoza maelfu ya wananchi katika mazishi
wa mwasisi wa chama cha TANU na baadaye Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Peter Kisumo yaliyofanyika katika Kijiji cha Kirongwe wilayani Mwanga
mkoani Kilimanjaro.
Ibada ya mazishi ilifanyika katika Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Pare ambako ibada ya mazishi
iliongozwa na aliyekuwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini, Dk. Marth
Shao.
Rais Kikwete aliwasili kijijini hapo saa 9:10 kwa kutumia helkopta
mbili ambazo zilitua kwa nyakati tofauti katika Uwanja wa Chuo cha
Ufundi (UVTC) Mwanga.
Hata hivyo, Rais Kikwete hakuzungumza chochote badala yake Waziri wa
Sheria na Katiba, Dk. Asha Rose Migiro, alizungumza kwa niaba ya CCM na
Serikali.
Dk Migiro alisema Kisumo aliishi maisha yaliyotukuka na kwa misingi ya maadili ya utumishi wa umma.
Alisema mzee Kisumo alikuwa mtu wa namna ya pekee ambaye katika ujana
wake alifanya kazi katika sekta mbalimbali kwa tija kubwa hivyo kifo
chake kimeacha pengo kubwa.
“Mzee Kisumo alikuwa mtumishi mahiri na muadilifu wa serikali na
aliteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali za juu serikalini na katika
chama cha TANU na baadaye CCM na aliweza kuandika Katiba ya mwaka 1977
pamoja na kujenga kada ya uongozi katika taifa,”alisema Dk. Migiro.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment