RAIA wa China, Jianfeng Wu amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka ya kukutwa na meno ya simba yenye
thamani ya Sh milioni 10.1.
Baada ya kusomewa mashitaka, mshitakiwa hakuruhusiwa kujibu mashitaka
kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo ya uhujumu
uchumi isipokuwa Mahakama Kuu.
Awali, wakili wa Serikali, Paul Kadushi alidai mbele ya Hakimu Mkazi
Mfawidhi, Cyprian Mkeha kuwa ilikuwa Agosti 18, mwaka huu katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Wu alipokamatwa akiwa na meno
matatu ya simba. Hakimu Mkeha aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 10,
mwaka huu itakapokuja tena mahakamani hapo kwa hatua nyingine.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment