Juhudi za uokozi wahamiaji 500 waliofariki baada ya mashua kuzama Mediterania zinaendelea.
Juhudi za uokoaji zinaendelea kwenye Pwani ya Libya baada ya boti mbili zilizokuwa zimebeba wahamiaji wapatao 500 kuzama karibu na bandari ya Zuwara.
Boti ya kwanza iliyoomba msaada kabla ya kuzama ilikuwa na watu 50 wakati boti ya pili iliyozama baadaye ilikuwa na watu 400 na mpaka sasa zaidi ya watu 20 wameokolewa, lakini mamia ya wengine hawajulikani waliko na wanahofiwa kufa-maji.
Taarifa ambayo haijathibitishwa inasema kuwa kuna kiasi cha miili 100 katika hospitali moja ya Zuwara ikiwemo ya watu kutoka Syria, Bangladesh na za jangwa la Sahara.
Katika kipindi cha mwaka huu zaidi ya wahamiaji elfu mbili wamekufa wakijaribu kwenda Ulaya kupitia Libya wakati wengine 160,000 wamefanikiwa kufika hasa Italia na Ugiriki.
0 comments:
Post a Comment