Iniesta kuchukua usukani wa Barcelona.
Kiungo wa Barcelona Andres Iniesta ameridhi unahodha wa timu hiyo kufuatia kuondoka kwa Xavi.
Iniesta amechaguliwa kuwa nahodha wa timu ta Barcelona kupitia mfumo wa uchaguzi ambapo wachezaji wa timu ya hiyo humchagua nahodha wao.
Mfumo huu ni tofauti na ule unaotumiwa na timu nyingi ambapo kocha humchagua nahodha wa timu.
Mfumo huu pia ulitumiwa kumchagua Xavi baada ya nahodha wa zamani Carles Puyol kustaafu.
Andres Iniesta atasaidiwa na Lionel Messi, Sergio Busquets na Javier Mascherano katika nafasi za msaidizi wa kwanza, pili na wa tatu mtawalia.
Msimu uliopita Iniesta alihudumu kama nahodha katika mechi nyingi ambazo nahodha Xavi hakuhusishwa.
0 comments:
Post a Comment