WIZARA ya Maliasili na Utalii imeanza kufanya uchunguzi kwa
kushirikiana na mamlaka mbalimbali, ikiwemo Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
(TAA) na vyombo vya ulinzi na usalama ili kubaini waliohusika na
upitishwaji wa nyara za serikali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA) hivi karibuni.
Wizara hiyo pia imeeleza kupokea kwa masikitiko makubwa taarifa hizo
za kukamatwa kwa nyara za serikali katika Uwanja wa Ndege wa Zurich
nchini Uswisi zikiwa njiani kwenda China kutokea Uwanja huo wa Ndege wa
Kimataifa wa JNIA wa jijini Dar es Salaam.
Taarifa ya wizara hiyo kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Waziri
Lazaro Nyalandu ilisema wizara hiyo inaupongeza uongozi wa Uwanja wa
Ndege wa Zurich na Serikali ya Uswisi na watu wote walioshiriki kubaini
na kukamata nyara hizo.
Kwa mujibu wa Waziri Nyalandu, nyara hizo zinajumuisha meno ya tembo
yenye uzito wa kilo 262, kucha na meno ya simba vyenye uzito wa kilo
moja. Alisema tukio la kukamatwa kwa nyara hizo lilitokea kwenye uwanja
huo Julai 6, mwaka huu zikiwa ndani ya masanduku manane zikiwa njiani
kwenda Beijing China kutokea uwanja wa ndege wa Dar es Salaam kupitia
Zurich.
“Wizara imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa hizi na kwamba nyara
hizo zimesafirishwa kupitia Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere. Tukio
hili linadhihirisha kuwa tatizo la ujangili bado linaendelea ndani na
nje ya nchi yetu” alisema.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment