Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akifafanua jambo kwa umakini mbele ya waandishi wa habari kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es
Salaam.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
MGOMBEA
mteule wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli, leo Jumanne
Agosti 4, 2015 atawasili Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kuchukua fomu ya
kuomba kugombea Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba Mwaka
huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema, msafara wa Dk. Magufuli kwenda kuchukua fomu hiyo, utaanza saa tano asubuhi ukitokea Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.
Nape amesema, msafara ambao utaambatana na shamrashamra za aina yake, utapita katika Barabara za Morogoro, Bibi Titi Mohammed na Ohio kabla ya kufika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi zilizopo Posta House, karibu na makao Makuu ya Jeshila Polisi.
Amesema, Dk. Magufuli ambaye ataambatana na Mgombeamwenza wake, Mhe. Samia Suluhu, mbali na makada, wapenzi na wanachama wa CCM,atasindikizwa na viongozi mbaimbali wakiwemo, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Dk. Magufuli alichaguliwa na Mkutano Mku wa CCM uliofanyika Oktoba 11, 2015, mjini Dodoma, baada ya kuwashinda wagombea wenzake, Dk. Asha-Rose Migiro na Balozi Amina Salum Ally.
Home
News
Mgombea mteule wa urais CCM,Dkt Magufuli kuchukua fomu tume ya taifa ya uchaguzi leo jumanne.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment