Msemaji wa serikali ya Marekani amesema kuwa Marekani inataka kuona mashambulizi ya kigaidi yakisitishwa.
Msemaji wa serikali ya Marekani Mark Toner amesema kuwa Marekani imesikitishwa na mashambulizi ya kigaidi yaliyofuata shambulizi la Suruch ambapo watu 32 walipoteza maisha.
Mashambulizi hayo yanayoaminika kutekelezwa na kundi la kigaidi la PKK yamelenga wanajeshi na maafisa wa polisi.
Wanajeshi 3 wameuawa huku wengine 28 wakijeruhiwa katika mashambulizi tofauti ya kigaidi.
Toner pia aligusia madai ya kuwa raia waliuawa katika mashambulizi yaliyotekelezwa na majeshi ya Uturuki Kaskazini mwa Irak.
Toner alisema kuwa raia hawafai kulengwa katika mashambulizi hayo.
0 comments:
Post a Comment