Wauguzi wanaofanya kazi katika hospitali za umma nchini kenya Wamekubali kusitisha mgomo uliochukua takriban miezi mitano na kurudi kazini leo saa kumi na moja jioni.
Katibu mkuu wa Muungano wa wauguzi -Knun- SETH PANYAKO amewataka wauguzi kurudi kazini mara moja.
Mwenyekiti wa magavana nchini Kenya JOSPHAT NANOK amesema kuwa makubaliano hayo na wauguzi yamefikiwa baada ya majadiliano makali.
Kulingana na makubaliano ,wauguzi wataanza kupokea marupuru ya nguo za kazini za ksh.15,000 kuanzia mwaka wa fedha cha 2018-2019.
Bwana NANOK amesema Marupurupu hayo yameongezeka kutoka 10,000 waliokuwa wakipata na pia yataendelea kuongezwa kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo baada ya kipindi cha bajeti cha 2018-2019.
Aidha amesema wauguzi hao wataanza kupokea marupurupu ya kuwa hatarini ya kati ya ksh.20,000 na ksh.25,000 za Kenya kulingana na kundi la kazi alioajiriwa katika kipindi cha bajeti ijayo.
Nanok amesema kuwa marupurupu hayo yataongezwa hadi ksh.30,000 katika kipindi cha bajeti cha 2020/2021.
Ameongezea kwamba baraza hilo la magavana limeondoa kesi zote dhidi ya wauguzi hao mahakamani mbali na kuahidi kwamba mishahara yote italipwa mwishoni mwa mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment