Hayo yamesemwa na wanaharakati
kutoka katika mashirika mbalimbali yanayotetea haki za binadamu wakati wa
kuzindua mpango mkakati wa elimu kwa njia ya filamu katika maeneo ya vijijini
huku wakiutaja mkoa wa shinyanga kuongoza kwa idadi ya ndoa na mimba za utotoni
hali inayochangia kurudisha nyuma jitihada kumkomboa mwanamke kielimu.
Aidha baadhi ya wasichana
walikumbwa na changamoto ya ndoa na mimba za utotoni wameelezea jinsi
walivyoadhirika kisaikolojia na hali hiyo huku wakiitaka serikali kushirikiana
na mashirika ya kutetea haki za mtoto wa kike kutoa elimu ya kutosha katika
maeneo ya vijijini ili kuikwamua jamii katika dhana ya mila na desturi potofu.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya
shinyanga mjini Bi.joaephine Matiro amekiri kuwa ndoa na mimba za utotoni ni
changamoto kubwa katika mkoa wa shinyanga huku akidai kuwa kuna haja ya kuweka
mikakati kati ya serikali na mashirika ya kutetea haki za binadamu kuhakikisha
hali hiyo inadhibitiwa kwa kupeleka elimu katika maeneo ya vijijini ili
kutokomeza mila na desturi potofu zinazochanigia vifo vya akina mama
wajawazito.
0 comments:
Post a Comment