Walemavu wa ngozi wakionekana hapo(Picha na Maktaba).
Mila na desturi za baadhi ya makabila nchini zinazowasukuma kuwaficha watoto wenye ulemavu bado zinatajwa kuwa tatizo linalokwamisha ustawi wa jamii ya kundi la watu hao wenye nafasi kubwa katika maendeleo ya taifa.
Wakizungumza kwenye kituo cha kuhudumia watoto wenye ulemavu wa aina mbalimbali cha Pluster kilichopo eneo la Ngaramtoni Wilayani Arumeru kikundi kimoja cha kinamama kilichofika kituoni hapo kutoa msaada wamesema ipo haja kwa jamii hiyo kubadilika katika kipindi hiki ambacho teknolojia ya kurekebisha ulemavu imekua.
Awali akizungumzia utoaji wa huduma kituoni hapo mlezi wa watoto wanaopatiwa huduma, Bi JOYCE MBISE amesema bado mazingira ya kuwapata watoto walengwa kwenye maeneo ya pembezoni ni magumu.
Hata hivyo inaelezwa kuwa kituo hicho cha huduma kwa walemavu kinachoratibiwa na Hospitali ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Seliani, kinakabiliwa na matatizo mbalimbali ambayo wadau wanatoa wito kwa jamii kutoliachia jukumu hilo kanisa peke yake.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment