Image
Image

Mkutano mkuu CHADEMA wawapitisha Lowassa na Duni Haji kupeperusha bendera ya Ukawa Mbio za Urais.


MKUTANO Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa pamoja wamempitisha kwa kishindo Edward Lowassa Waziri Mkuu mstaafu kuwa mgombea urais kupitia Chadema na Umoja wa Katiba Ukawa.
Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Mlimani city Jijini Dar es Salaam leo umempitisha Mgombea mwenza Juma Duni Haji katika kura zilizopigwa kwa kanda kuulizwa na Mwenyekiti wa Taifa Chadema Freeman Mbowe.
Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo chademaMh.Freeman Mbowe amesema kuwa wakati huu ambao wanapigania ukombozi wa kweli kwa taifa ni lazima kukubali kuwa umoja walio nao bila ya kutenganishwa na misingi ya Ukabila wala Udini wanawahitaji watanzania wote kuwa kitu kimoja ili kutekeleza ndoto ya taifa hili la Tanzania katika kuleta mabadiliko ya kweli.
Mbowe amesema kuwa Mabadiliko kamwe hayawezi kuja yenyewe bila ya Mabadiliko yanaletwa kwa kila mmoja kujitoa kwani anasema wamepigana kwa takribani miaka 25,watu wamepoteza maisha,wengine kubaki na ulemavu hiyo yote ilikuwa ni kwaajili ya kutetea wanyonge katika taifa hili.
Amesema siku zote katika kutafuta haki na kuweka usawa kwa walicho nacho na wasio nacho huwa inahitaji uvumilivu mkubwa kwani vyama vyote vya UKAWA vimepitia milima na mabonde ili tu kuhakikisha kwamba uwiano unakuwa sawa kwa kila mmoja na haswa kwa kipindi hiki ambapo wanaenda kuishika dola niwakati wa watanzania kuendelea kuwa na imani na Muunganiko wa vyama hivyo ili kuleta matumaini mapya,fikra mpya na mtizamo mpya wenye ukombozi katika taifa na watanzania wenyewe.

Amesema hakuna mtu wala chama kisicho kuwa na Mapungufu lakini yakizidi sana inabidi kumpumzika ili usaidiwe kwani itakuwa umechoka hivyo kama chadema na wao wanamapungufu yao lakini katika kuleta mabadiliko ya kweli katika taifa hili uzalendo na uthubutu wenye manufaa haswa kwa kuona walivyo waasisi wa taifa hili sasa ni wakati wa Ukawa kuchukua nchi na kuleta mtizamo wenye matumaini ya kweli katika Taifa.

Mh.Mbowe amebainisha kuwa ushirika wao unamaana kama walivyokubaliana kwenye UKAWA kwamba wawe na mgombea mmoja wa urais katika mchakato huo na kwenye udiwani ili kuwepo na usawa na kusema kuwa kwani ni faraja kwa kuwa kaika mchakato huo wameanza na mungu na watamaliza na mungu katika utendaji wa miujiza na anatenda kwa ajili ya chama hicho kwa makusudi na sio kwa bahati mbaya ili kulijenga taifa.

Mh.Mbowe amewahakikishia watanzania kuwa sasa UKAWA unachukua nchi na safari hii ni safari ambayo ni ya uhakika na isiyo rudi kamwe ambapo Mtu wanaye msimamia kupeperusha bendera ni kipenzi cha watu wote nchini,Imani ya Mh.Edward Lowassa kupeperusha bendera ya chama Cha CHADEMA kupitia umoja wa Katiba ya wananchi ukawa  ni wenye kuungwa mkono wa hali ya juu ndani ya chama hicho ambapo aliyekuwa makamu mwenyekiti wa CUF na waziri wa Afya Duni Haji,amelazimika Kujiuzulu Uwaziri wa Zanzibar na Umakamu wa Wananchi CUF ili kuweza kuwa mgombea mwenza wa UKAWA ili kuleta ushindi kwa chama hicho na umoja huo wa ukawa kwa ujumla.

Mbowe amesema Tanzania ina ndoto ya mabadiliko ambayo inachagizwa na kazi kubwa iliyofanywa na viongozi na wanachama wa Chadema wakiwemo CUF, NLD na NCCR Mageuzi.
CHADEMA imewapokea rasmi na kuwakabidhi kadi viongozi kadhaa mashuhuri waliokuwa CCM na ambao wamejiunga na CHADEMA.Wamekabidhi kadi viongozi wanne wanaowakilisha makundi kadhaa yaliyojiorodhesha kujiunga CHADEMA.Kadi ya kwanza imetolewa kwa Mgana Msindai Mwenyekiti wa Wenyeviti wa mikoa wa CCM akiwakilisha wenyeviti kadhaa walioomba kujiunga CHADEMA.Kadi ya pili amekabidhiwa Makongoro Mahanga Naibu Waziri wa Kazi na Ajira kwa niaba ya mawaziri na manaibu waziri kadhaa walioomba kujiunga na jeshi la ukombozi.Kadi ya tatu imetolewa kwa Mbunge wa Arumeru Magharibi Ole Madeye akiwakilisha wabunge wengi walioomba kujiunga CHADEMA.Kadi ya nne imetolewa kwa Katibu wa fedha na Uchumi CCM Kahama ambaye anawakilisha viongozi wa wilaya kwa mamia ambao mpaka sasa wameorodhesha majina yao ili wasimame wahesabiwe!

Endelea kusoma taarifa zetu tutakuletea kwa kina habari hii.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment