Mkuu wa wilaya ya muleba mkoani kagera,Francis Isaac,amepandishwa kizimbani, mbele ya baraza la ardhi na nyumba, wilaya ya Singida, akidaiwa kupora kiwanja cha mjane mmoja, kilichopo katika mtaa wa minga, manispaa ya Singida.
Issac ambaye aligombea
ubunge,jimbo la mkalama,mkoani Singida na kuambulia nafasi ya tatu wakati wa
zoezi la kura za maoni Agosti Mosi mwaka huu, katika madai hayo, ameunganishwa
na shekhe mmoja aliyetajwa kwa jina la Salumu Rajabu Sima.
Mbele ya baraza hilo,
mwenyekiti Saidi Wambili amesema kuwa, juni 15, 2012, mlalamikiwa isaac kwa
kushirikiana na Shekhe Sima, walikula njama ya kuchukua kiwanja namba 116,
kitalu ‘s’, mali ya amina Abdallaha (80), bila ya kibali chochote kisheria.
Katika hati yake ya
madai, amina ambaye ni msimamizi wa mirathi ya marehemu mumewe, Kilawe Nchomba,
analitaka baraza hilo liwaamuru walalamikiwa hao, kumlipa sh.milioni nane,
ikiwa ni fidia ya kubomoa jengo lililokuwemo awali, kwenye kiwanja hicho.
Amina pia ameliomba
baraza hilo liwazuie walalamikiwa hao kuingia ndani ya kiwanja hicho, waache
kukiendeleza na baraza limtangaze yeye (amina) kuwa ndiye mmiliki halali wa
eneo hilo.
Mapema akitoa ushahidi,
Ofisa ardhi manispaa ya Singida, Gaudence Mwakalomba amesema ,awali
kiwanja hicho kilimilikiwa na Kilawe nchomba, lakini baadaye sima alikihamisha
kinyemela hadi kwa Francis Isaac, bila ya kufuata taratibu.
Hata hivyo shauri hilo
namba 32 la mwaka 2013, linasikilizwa na baraza bila ya walalamikiwa kuwepo,
kutokana na kupuuza amri ya baraza hilo kuwataka wahudhurie limeahirishwa
0 comments:
Post a Comment