KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars Charles Mkwasa
ameita kikosi cha wachezaji 29 kwa ajili ya kambi ya Uturuki huku
wachezaji tisa wakitoka Azam.
Stars inatarajiwa kwenda kuweka kambi ya wiki mbili Uturuki kujiandaa
na mechi ya kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa Afrika dhidi ya
Nigeria itakayochezwa nchini Septemba 5 mwaka huu. Miongoni mwa
wachezaji tisa wa Azam, yumo kinda Farid Mussa aliyefunga bao
lililoipeleka timu hiyo kwenye fainali kwenye mechi dhidi ya KCCA ya
Uganda.
Akitangaza kikosi hicho kitakachoingia kambini keshokutwa kocha
Mkwasa, aliweka wazi kuwa wameangalia wachezaji kwenye mashindano ya
Kagame, ambayo yamemalizika hivi karibuni.
“Kikosi hiki cha wachezaji 29 kitaingia kambini siku ya Jumapili
katika hoteli ya Tansoma iliyopo Gerezani kwa ajili ya kambi ya wiki
moja ya mazoezi kabla ya kwenda kuweka kambi ya siku kumi jijini
Istanbul - Uturuki, ambapo itacheza michezo miwili ya kirafiki na timu
za Taifa za Libya na Kuwait kabla ya kurejea nchini kuwavaa Nigeria,”
alisema Mkwasa.
Katika kikosi hicho Mkwasa amewajumuisha wachezaji watano wanaocheza
soka la kulipwa nje ya nchi ambao baadaye watajumuika kwa kambi ya
kujiandaa kucheza na Nigeria, Septemba 2015 nchini Uturuki.
Wachezaji walioitwa ni magolikipa, Ally Mustafa (Yanga SC) na Aishi
Manula (Azam FC), walinzi wa pembeni: Shomari Kapombe (Azam FC), Michael
Aidan (Ruvu Shooting), Juma Abdul, Mwinyi Haji (Yanga SC) na Abdi Banda
(Simba SC).
Walinzi wa kati; Hassan Isihaka (Simba SC), Nadir Haroub, Kelvin
Yondani (Yanga SC), Viungo wakabaji: Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir
Yahya (Azam FC), Viungo washambuliaji ni Salum Telela (Yanga SC) na Said
Ndemla (Simba SC).
Washambuliaji wa pembeni: Orgenes Mollel (Aspire – Senegal),
Abdrahman Mbambi (Mafunzo), Deus Kaseke, Saimon Msuva (Yanga SC),
Ramdhani Singano, Farid Musa (Azam FC), huku washambuliaji wa kati
wakiwa ni John Bocco, Ame Ally (Azam FC) na Rashid Mandawa (Mwadui FC).
Wachezaji wa kimataifa waliojumuishwa katika kikosi hicho ambacho
Agosti 23 kitaelekea kambini nchini Uturuki kwa kambi ya siku kumi ni
Mbwana Samata, Thomas Ulimwengu (TP Mazembe – DR Congo), Mrisho Ngasa
(Free State - Afrika Kusini) na Hassan Sembi (Santos FC – Afrika Kusini)
na Adi Yussuf (Mansfield Town – Uingereza.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment