YANGA imemsajili beki wa kati Vincent Baossou kutoka Togo kuziba nafasi ya Joseph Zuttah wa Ghana aliyetupiwa virago.
Tayari Bossou yuko nchini na inaonekana ameridhia kujiunga na Yanga
ambayo inataka kuimarisha safu ya ulinzi iliyoonekana kupwaya katika
michuano ya Kagame iliyoishia hatua ya robo fainali.
Beki huyo alianza soka lake kwenye klabu ya Maranatha FC mwaka 2006
na kudumu kwenye klabu hiyo mpaka mwaka 2009 akicheza jumla ya mechi 77
na kuifungia klabu hiyo magoli matano (5).
Alijiunga na klabu ya Etoile Sportive du Sahel, Januari 2010 kwa
mkataba wa miaka miwili lakini mkataba wake ukavunjwa baada ya miezi
mitatu baadaye akiwa ameichezea klabu hiyo mechi tatu tu, na karudi tena
Maranatha FC Machi 18, 2010.
Mei 2011 alijiunga na klabu ya Navibank Saigon F.C ya Vietnam ambapo
alicheza mechi 35 na kufanikiwa kufunga mabao matatu na kwa sasa alikuwa
na mkataba na klabu ya Govang Hi FC ya Korea Kusini.
Pia Bossou alikuwepo kwenye kikosi cha Togo ambacho kilijitoa
kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika 2010 baada ya basi la timu hiyo
kushambuliwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni magaidi wakati wakielekea
Angola ilipofanyika michuano hiyo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment