TANZANIA imeendelea kufanya vibaya kwenye nafasi ya ubora wa viwango
vya Fifa na sasa imeporomoka mpaka nafasi ya 140 kutoka 139 mwezi
uliopita.
Timu ya soka ya taifa, Taifa Stars imekuwa ikifanya vibaya tangu
kuanza kwa mwaka huu hali iliyofanya Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la
soka Tanzania (TFF) imfute kazi kocha Mholanzi Mart Nooij na mikoba
yake kupewa mzawa Charles Mkwasa.
Kwa mujibu wa viwango hivyo, timu za ukanda wa Afrika Mashariki na
Kati ambazo ni wanachama wa Baraza la vyama vya soka kwa ukanda huo
(Cecafa) zimezidi kuwa taaban kulinganisha na timu za Kusini zinazofanya
vizuri kila kukicha.
Timu zilizo chini ya Cecafa zilizo kwenye ‘ahueni’ kidogo ni Uganda
inayoshika nafasi ya 74, Sudan ya 87, Rwanda ya 91, Ethiopia ya 99,
Kenya ya 116 na Burundi ya 132.
Sudan Kusini ipo nafasi ya 195, Eritrea ya 203, Somalia ya 204 na
Djibouti ni ya 206. Viwango hivyo vimetoka Stars ikijiandaa kumenyana na
Nigeria mechi ya kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa Afrika
mwaka 2017 Septemba 5 mwaka huu. Wapinzani hao wa Stars Nigeria wapo
katika nafasi ya 53.
Aidha wapinzani wengine wa Stars kwenye kuwania michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 Malawi wameshika nafasi ya 98
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment