Mgombea ubunge jimbo la Kishapu kupitia Ukawa ndugu Fred Mpendazoe
akizungumza na wakazi wa Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine
aliwataka watanzania kukubali mabadiliko kwani CCM imechoka huku
akisisitiza kuwa mgombea urais wa CCM John Magufuli hana kabila zaidi ya
kabila la CCM ambayo kamwe haiwezi kutoa rais bora
Mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi
akiwahutubia wakazi wa Shinyanga ambapo alisema pamoja na hujuma
anazofanyiwa na baadhi ya watu wakiwemo wafuasi wa CCM akiwemo mgombea
ubunge wa CCM jimbo hilo Stephen Masele hatakata tamaa kuwapigania haki
wananchi na kwamba yuko tayari kufa kwa ajili ya wananchi
Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa na Uenezi kanda ya ziwa Chadema Juma
Protas akizungumza katika mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni ambapo
aliwasisitiza wananchi kuchagua viongozi wa Ukawa ambayo ndiyo
mwarobaini wa maendeleo ya watanzania
Mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Msalala Paul Malaika akizungumza
na wakazi wa Shinyanga ambapo alisema hata kama kuna mgombea mwenye sifa
nzuri ndani ya CCM wananchi wasimchague kutokana na kwamba mfumo mzima
wa CCM ni mbovu hivyo wafanye mabadiliko kwa kuiweka Ukawa madarakani
Mheshimiwa James Lembeli na fimbo yake ya kimila akimsikiliza kwa
umakini zaidi mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi.
Mheshimiwa James Lembeli akimwombea kura mgombea urais wa Ukawa
mheshimiwa Edward Lowassa na mgombea ubunge jimbo la Shinyanga Patrobas
Katambi kwa wakazi wa Shinyanga.
Wakazi wa Shinyanga wakiwa katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga
wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za Ukawa/Chadema katika jimbo
la Shinyanga
Makamanda wa Ukawa wakiwa meza kuu
Wagombea udiwani kupitia Ukawa katika kata 17 za manispaa ya Shinyanga wakitambulishwa wakati wa mkutano huo.
Maelfu ya wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la mkutano.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment