Mwalimu huyo anayefunza katika shule ya msingi ya Mohei
iliyoko mjini Zhaotong, alikamatwa na polisi baada ya kuripotiwa na wakazi wa
eneo hilo.
Mnamo tarehe 29 mwezi Julai, polisi
walifikishiwa mashtaka na mmoja wa wakazi wa mji alitoa madai ya kubakwa kwa
binti yake na mwalimu huyo wa shule.
Taarifa hiyo ilizua utata kwa wakazi
wa mji na kudai kwamba mwalimu huyo alitekeleza kitendo hicho kichafu
kwa wanafunzi wengi wa kike wanaosoma katika shule hiyo.
Wengi wa wanafunzi
waliokumbwa nam kasa huo wanasemekana kuishi majumbani mwao na jamaa wao wa
karibu huku wazazi wao wakiishi na kufanya kazi katika miji mikubwa nchini China.
Uchunguzi kuhusiana na kesi hiyo
bado unaendelea kufanyika nchini humo.
0 comments:
Post a Comment