Vikosi vya usalama nchini Somalia vimeripotiwa kumuangamiza mmoja wa wanamgambo wa kundi la Al-Shabaab waliopanga kutekeleza shambulizi kwenye gereza moja lililoko mjini Hiran.
Afisa mkuu wa vikosi vya usalama Mohamed Noor, alitoa maelezo kwa vyombo vya habari na kusema kwamba kundi la Al-Shabaab lilikuwa limepanga kushambulia gereza hilo mapema leo hii.
Vikosi vya usalama vilikabiliana na wanamgambo hao kabla ya kutekeleza shambulizi hilo na kufanikiwa kumuua mmoja wao.
Wakazi wa eneo hilo waliarifu kuamshwa usingizi kwa milio ya risasi ingawa makabiliano hayo hayakudumu kwa muda mrefu.
Licha ya kundi la Al-Shabaab kupoteza baadhi ya maeneo waliyokuwa wakiyadhibiti nchini Somalia, wanamgambo wa kundi hilo bado wanaonekana kuendeleza mashambulizi mara kwa mara.
0 comments:
Post a Comment