Jeshi la Polisi nchini
limesitisha maandamano ya aina yoyote wakati wote wa zoezi la kuchukuwa fomu,kutafuta
wadhamini mikoani na hata wakati wa kurejesha fomu ili kuweka hali ambayo
haitaleta usumbufu au kuhatarisha usalama wa raia na mali zao.
Akitoa taarifa hiyo mbele ya
waandishi wa habari jijini Dar es Dalaam Naibu Inspekta Jenerali wa polisi
Abdulrahiman Kaniki uamuzi huo umefikiwa baada ya jeshi hilo kupokea malalamiko
kutoka kwa wananchi juu ya usumbufu uliojitokeza wa watu kushindwa kuingia
maofisini na wengine kushindwa kufika kwa wakati katika shughuli za kiuchumi na
kijamii kutokana na misafara mirefu iliyosababishwa na vyama vya CHADEMA na CCM
wakati wagombea wao walipokwenda kuchukuwa fomu.
Aidha amesema jeshi hilo halina
ugomvi na chama chochote cha siasa wala mchakato wa uchaguzi unaoendelea
isipokuwa lengo lao ni kutengeneza mazingira mazuri ili vyama vyote viweze
kutekeleza majukumu yao vizuri na kwa kufuata sheria za nchi.
0 comments:
Post a Comment