Image
Image

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini CAR ajiuzulu kufuatia madai ya kubakwa kwa mtoto wa miaka 12.


Mwakilishi wa UN katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati (CAR) Babacar Gaye amejiuzulu kufuatia madai ya kubakwa kwa mtoto wa miaka 12 na walinda usalama wa UN. Madai haya yaliwasilishwa wakati ambapo kikosi cha kulinda usalama kinalaumiwa kwa kumuua mwana na babake walipofyatua kiholela holela katika mtaa mmoja nchini humo.
Mshauri wa shirika la Amnesty International Joanne Mariner alisema, “Jopo huru linafaa kuundwa ili kuchunguza madai hayo na kila atakayepatikana na hatia anafaa kuchukuliwa hatua.”
Akifahamisha kuwa Gaye aliwasilisha ombi la kujiuzulu Katibu Mkuu wa UN Ban Ki-Moon alisema kuwa janga hili limeenea kuliko kisa kimoja au kikosi kimoja cha usalama. Ban Ki-Moon alikiri kuwa Umoja wa Mataifa inafaa kutafuta suluhisho la matukio kama haya ambayo yamekuwa janga la kimataifa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment