Image
Image

Pluijm amesema timu yake bado haijaiva kiasi cha kuridhika kutetea taji lake la Ligi Kuu.

KOCHA Mkuu wa Yanga Hans van der Pluijm amesema timu yake bado haijaiva kiasi cha kuridhika kutetea taji lake la Ligi Kuu hivyo inahitajika marekebisho kidogo.
Yanga ipo Mbeya kujiandaa na mechi ya ngao ya jamii dhidi ya Azam itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam Agosti 22 mwaka huu.
Katika maandalizi ya mechi hiyo, juzi ilicheza mechi ya kirafiki na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya na kushinda mabao 2-0.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Mbeya jana, kocha Pluijm alisema kikosi chake kipo vizuri lakini bado hajaridhika nacho.
“Tunafanya maandalizi ya kutetea taji letu la ligi, timu yangu sio mbaya lakini kuna vitu sijaridhika navyo nataka kurekebisha,” alisema.
Hata hivyo hakusema ni vitu gani, lakini huenda moja ya jambo analotaka kufanya marekebisho ni kwenye ushambuliaji.
“Timu yangu imecheza mechi mbili za kirafiki tangu tuje huku (Mbeya) na Kimondo na Prisons kuna vitu nimeviona nataka kuvifanyia kazi,” alisema.
Aliongeza pia, suala la ubovu wa viwanja vya mikoani limekuwa tatizo kwa timu yake na kwamba anafanya maarifa ya kuona timu yake icheze vipi linapofika kwenye mechi za mikoani.
“Kuna tofauti kubwa ya timu ikicheza mechi Dar na mikoani kwa maana viwanja vingi vya mikoani huwa havina ubora vinabadilisha hali ya mchezo,” alisema.
Yanga ilicheza na Kimondo mjini Mbozi na kuifunga mabao 4-1 kabla ya kuifunga Prisons mabao 2-0, keshokutwa inatarajia
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment