Na Bakari Kimwanga, Dodoma
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekamilisha uteuzi wa wagombea ubunge wa
majimbo na viti maalumu, huku baadhi ya wagombea walioshinda kwenye
kura za maoni wakiachwa na kuchukuliwa walioshika nafasi ya pili na ya
tatu.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema kukamilika kwa kazi hiyo kunatoa
fursa kwa wana CCM kujipanga na kuhakikisha wanarudisha umoja na
mshikamano ili chama kiweze kushinda uchaguzi katika ngazi zote.
Alisema pamoja na hali hiyo uteuzi huo wa wagombea wa nafasi
mbalimbali umezingatia uwezo wa mwanachama kukubalika kwa jamii pamoja
na chama na kura za maoni haikuwa kigezo pekee cha uteuzi, ila vikao vya
uteuzi huangalia sifa za ziada kwa mujibu wa utaratibu na kanuni za
CCM.
Katika Jimbo la Handeni Vijijini, kikao hicho kimemteua Makamu
Mwenyekiti wa UVCCM ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mufundi mkoani
Iringa, Mboni Mhita aliyekuwa mshindi wa pili na kumwacha John Salu
ambaye ushindi wake ulionekana kuwa na matatizo.
Kwa upande wa viti maalumu, Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki,
Angella Kizigha, alijikuta akikubwa na kimbunga hicho kwa jina lake
kukatwa, ambapo mshindi wa pili amekuwa wa kwanza na wa tatu amekuwa wa
pili.
Mbali na huyo pia mtoto wa aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam,
ambaye pia ni mgombea ubunge Jimbo la Ubungo Dk. Didas Masaburi naye
amekumbwa na panga la NEC.
Mtoto huyo wa Masaburi, Juliana Masaburi, ambaye alishinda kura za
maoni kupitia kundi la vijana akiwakilisha Mkoa wa Mara amekatwa na
badala yake nafasi yake imechukuliwa na msanii maarufu wa Bongo Move,
Irene Uwoya.
“Tumemaliza vizuri kazi ya uteuzi wa wagombea wa nafasi za ubunge wa
majimbo viti maalumu, uwakilishi na uwakilishi viti maalumu. Kuna baadhi
ya majimbo NEC tumefanya uteuzi kwa mtu wa pili na wa tatu na kuwateua
kutokana na sababu mbalimbali.
“Na yapo baadhi tumerudia uchaguzi na hata kwingine kurudiwa
kuhesabiwa kura upya ambapo hadi sasa hayo majimbo mchakato wake
utakamilika Agosti 17, mwaka huu ambapo Kamati Kuu Maalumu itakutana na
kufanya uteuzi wa mwisho,” alisema Nape.
Majimbo ambayo uteuzi umefanyika ni pamoja na Mkoa wa Arusha na
majimbo yao katika mabano ni Philemon Mollel (Arusha Mjini), Dk. Wilbard
Slaa Lorri (Karatu), Loy ole Sabaya (Arumeru Magharibi), John Sakaya
(JD) (Arumeru Mashariki), Dk. Stephen Kiruswa (Longido), Namelock
Sokoine (Monduli) na William ole Nasha (Ngorongoro).
Dar es Salaam
Jimbo la Ukonga, kura zinarudiwa, Ilala Mussa Zungu, Bonna Kaluwa
(Segerea), Abasi Mtemvu (Temeke), Dk. Faustine Ndugulile (Kigamboni),
Issa Mangungu (Mbagala), Kippi Warioba (Kawe), Dk. Didas Masaburi
(Ubungo), Dk. Fenella Mukangala (Kibamba) pamoja na Iddi Azzan
(Kinondoni).
Dodoma
Katika Mkoa wa Dodoma walioteuliwa ni Juma Nkamia (Chemba), Omar
Badwel (Bahi), George Simbachawene (Kibakwe), George Lubeleje (Mpwapwa),
Livingstone Lusinde (Mtera), Antony Mavunde (Dodoma Mjini), huku Jimbo
la Chilonwa kura zikirudiwa.
Wengine ni Job Ndugai (Kongwa), Sanda Edwin (Kondoa Mjini) na Dk. Ashatu Kijaji (Kondoa Vijijini).
Geita
Walioteuliwa ni Costantine Kanyansu (Geita Mjini), Joseph Kasheku
(Geita Vijijini), Lolensia Bukwimba (Busanda), Augustino Massele
(Mbogwe), Dotto Biteko (Bukombe) huku mrithi wa Dk.John Magufuli ambaye
kwa sasa ni mgombea urais wa CCM ni Dk. Medard Kalemani (Chato) na
Hussein Amar (Nyangwale).
Kagera
Walioteuliwa ni Balozi Khamis Kagasheki (Bukoba Mjini), Jasson
Rweikiza (Bukoba Vijijini), Osca Mkasa (Biharamulo), Innocent Bashungwa
(Karagwe), Innocent Bilakwate (Kyerwa), Charles Mwijage (Muleba
Kaskazini), Profesa Anna Tibaijuka (Muleba Kusini), Dk. Diodorus Kamala
(Nkenge) na Alex Gashaza (Ngara).
Iringa
Kwa upande wa Mkoa wa Iringa ni Fredrick Mwakalebela (Iringa Mjini),
Williaam Lukuvi (Isimani), Godfrey Mgimwa (Kalenga), Kilolo (Kura
zinarudiwa), Mahmoud Mgimwa (Mufindi Kaskazini), Mendrad Kigola
(Mufindi Kusini) na Cosato Chumi (Mafinga Mjini).
Katavi
Walioteuliwa ni Sebastian Kapufi (Mpanda Mjini), Mos Kakoso (Mpanda
Vijijini), Issack Kamwele (Katavi), Richard Mbogo (Nsimbo) na Dk.
Pudenciana Kikwembe (Kavuu).
Kigoma
Walioteuliwa ni Christopher Chiza (Buyungu), Atashasta Nditye ambaye
alikuwa mshindi wa tatu (Muhambwe), Daniel Nsanzugwanko (Kasulu Mjini),
Augustino Holle (Kasulu Vijijini), Albert Ntabaliba (Manyovu), Amani
Kabourou (Kigoma Mjini), Peter Serukamba (Kigoma Kaskazini), Hasna
Mwilima (Kigoma Kusini).
Kilimanjaro
Katika uteuzi huo NEC imewateua, Danstan Mallya (Hai), Aggrey Mwanri
(Siha), Davis Mosha (Moshi Mjini), Profesa Jumanne Maghembe (Mwanga),
Anne Kilango Malecela (Same Mashiriki), David Mathayo (Same
Magharibi), Dk. Cyril Chami (Moshi Vijijini), Innocent Shirima
(Vunjo), Sanje Colman (Rombo).
Lindi
Walioteuliwa kuwania ubunge kupitia CCM ni Kassim Majaliwa (Ruangwa),
Faith Mitambo (Liwale),Hassan Masala (Nachingwea) Nape Nnauye (Mtama),
Said Mtanda (Mchinga), Hassan Kaunje (Lindi Mjini), Hasnain Dewji (Kilwa
Kusini), Murtaza Mangungu (Kilwa Kaskazini).
Manyara
Hali ilikuwa tofauti kwa wagombea wa majimbo ya Babati Mjini na
Vijijini ambapo wajumbe wa NEC waliponga kukatwa na wagombea hao na
kutaka warejeshwe katika kinyng’anyiro ambapo nafuu ikapatikana kwao
Kisyeri Chambiri (Babati Mjini), Jittu Vrajilal Son (Babati Vijijini),
Dk. Mary Nagu (Hanang’), Kiteto (Litaamuliwa na Kikao Kijacho cha Kamati
Kuu), Zacharia Issaay (Mbulu Mjini), Fratei Massay (Mbulu Vijijini),
Christopher Ole Sendeka(Simanjiro).
Mbeya
Sambwee Shitambala (Mbeya Mjini), Oran Njeza (Mbeya Vijijini), Haroon
Mullah(Mbarali), Sauli Amon (Rungwe), Atupele Mwakibete (Busokelo),
Janeth Mbene (Ileje), Weston Zambi (Mbozi), Ngailonga Kasunga (Vwawa),
Luca Siyame (Momba), Frank Mastara Sichalwe (Tunduma), Victor
Mwambalaswa (Lupa) na Philip Mulugo(Songwe).
Mbali na hilo pia alisema katika jimbo la Singida Mashariki ambalo
linaongozwa na Tundu Lissu (Chadema), matokeo yake yamefutwa na mchakato
utaanza upya ndani ya CCM kwa wagombea kuchukua fomu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment