Image
Image

Stewart Hall akiri kuumizwa kichwa na Washambuliaji wake.

KOCHA Mkuu wa timu ya Azam FC Stewart Hall amesema kuwa atalifanyia kazi suala la umaliziaji wa washambuliaji wake ambalo wamelionesha katika mechi ya kirafiki kati yake na KMKM juzi.
Stewart aliyasema hayo juzi baada ya kumalizika mchezo wa kirafiki kati yake na timu ya KMKM ambapo mabingwa hao wa Kombe la Kagame walishinda kwa bao 1-0.
Alisema kuwa katika mchezo huo wachezaji wake wametengeneza nafasi nyingi lakini walishindwa kuzitumia kutokana na umaliziaji kuwa mbovu.
Alisema kuwa amefurahishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake katika mchezo huo licha ya kupoteza nafasi nyingi.
“Wachezaji wametengeneza nafasi nyingi za kushinda lakini umaliziaji wao ulikuwa mbovu, tatizo ambalo nitalifanyia kazi,” alisema.
Kwa upande wake Kocha wa timu ya KMKM Ali Bushiri alikiri kuzidiwa kila idara.
Alisema kuwa Azam FC ni timu kubwa kwa kila kitu jambo ambalo huwezi kulilinganisha na timu yake, lakini anashukuru kuwa timu yake imepata mazoezi.
Katika mchezo huo Azam FC bao lake la pekee liliwekwa kimiani na mchezaji wake Kamagi Gadier katika dakika ya 18 ya mchezo huo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment