Image
Image

News Alert:Ugonjwa wa figo watajwa kuwa tishio Tanzania.


Zaidi ya madaktari bingwa 80 wa magonjwa ya figo kutoka nchi za Kenya,Burundi,Ujerumani,Italia na Tanzania wamesema Tanzania ni miongoni mwa nchi za kusini mwa jangwa la sahara zenye idadi kubwa ya wagonjwa wa figo kutokana na kuwa na madaktari bingwa kumi tu nchi nzima huku gharama za matibabu ya ugonjwa huo pia zikiwa za juu.
Rais wa chama cha madaktari bingwa wa figo Tanzania Dk. Onesmo Kisanga ameyasema hayo wakati wa mkutano mkuu wa pili wa mwaka wa chama hicho unaofanyika jijini Mwanza kwa lengo la kujadili magonjwa ya figo yanayojitokeza kwa wananchi, namna ya matibabu ya ugonjwa huo kwa kutumia teknolojia ndogo iliyopo kama nchi inayoendelea na kuwasilisha mrejesho juu ya tafiti mbalimbali zinazohusiana na magonjwa ya figo.

Naye mkurugenzi mkuu wa hospitali ya rufaa Bugando,mwanza Prof. Kien Mteta amesema utafiti uliofanywa na daktari bingwa wa magonjwa ya figo na kisukari Dk.Mubaraka Janmohammed mwaka 2011 na 2012, kwa wagonjwa wa kisukari katika hospitali ya rufaa Bugando ulionyesha kuwa zaidi ya asilimia 80 ya wagonjwa hao  waliohudhuria kwenye kliniki ya hospitali hiyo walikuwa na madhara ya ugonjwa wa figo.

Awali akifungua mkutano huo unaofanyika kwa siku mbili,mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo amewashauri wananchi kupima afya zao mara kwa mara na kuepuka kutumia dawa za miti shamba kwa madai kwamba zikitumika bila uangaifu zinaweza kusababisha madhara kwenye figo, magonjwa mengine yanayoweza kusababisha ugonjwa wa figo ni shinikizo la damu, ugonjwa wa kisukari na Ukimwi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment