Baraza la Usalama la UN latoa ripoti inayodhihirisha kutumika kwa silaha za Israel nchini Sudan Kusini.
Baraza la Usalama la UN, liliunda kamati maalum ya uchunguzi kuhusiana na silaha zinazotumika nchini Sudan Kusini.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na baraza hilo tarehe 21 mwezi Agosti, ilibainishwa kwamba silaha zinazotumika Sudan Kusini kuwa zimeundwa na shirika la silaha la Israel (IWI).
Ripoti hiyo iliyowasilishwa baada ya muda wa wiki 10 za uchunguzi, iliambatanishwa na picha za silaha zilizothibitisha ukweli wa madai hayo.
Wakati huo huo, baadhi ya silaha zilizokuwa mikononi mwa makundi ya waasi wa Sudan Kusini zilidaiwa kuundwa na shirika la China.
Maelezo zaidi ya ripoti hiyo yanaarifu kwamba baadhi ya silaha hizo huenda ikawa zilipelekwa nchini Sudan Kusini kabla ya mapigano.
Sudan Kusini imekuwa ikikumbwa na mapigano ya kikabila kwa kipindi cha zaidi ya miezi 20 tangu kuibuka kwa mzozo kati ya rais wa nchi Salva Kiir na makamu wake wa zamani Riek Machar.
0 comments:
Post a Comment