Rais wa Uturuki amuondolea mfungwa mmoja hukumu yake kutokana na matatizo ya kiafya.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan, amefutilia mbali hukumu ya mfungwa mmoja aliyehukumiwa kifungo cha miaka 6 na miezi 8 gerezani kutokana matatizo ya kiafya.
Uamuzi huo uliotolewa na rais Erdoğan ulichapishwa rasmi kwenye gazeti la serikali.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa, rais Erdoğan anaarifiwa kutia saini uamuzi wa kufutiliwa mbali kwa hukumu iliyobakia ya mfungwa huyo baada ya ripoti yake ya afya kudhihirisha hali mbaya aliyokuwa nayo.
Uamuzi huo ulikubaliwa na kutekelezwa kwa kuzingatia kifungu cha 104 cha katiba ya Uturuki.
Mfungwa huyo kwa jina la Ömer Demirkirişçil mwenye umri wa miaka 35, alihukumiwa na mahakama ya Konya kwa mauaji ya mtu mmoja na kumjeruhi mwingine mnamo tarehe 20 Oktoba 2009.
0 comments:
Post a Comment