Image
Image

News Alert:Uharibifu wa Mazingira wahatarisha hifadhi ya KISAMPA.

Kuendelea kuongezeka kwa vitendo vya ujangili,ukataji wa miti hovyo pamoja na kasi ya kuingiza mifugo katika hifadhi ya KISAMPA iliyopo katika kijiji cha Gongo Bagamoyo mkoani Pwani imeelezwa kuwa ni miongoni mwa sababu ambazo zinasababisha kutishia kutoweka kabisa kwa hifadhi.

Hayo yamebanishwa na baadhi ya viongozi wa serikali ya kijiji hicho wakati wa ukaguzi maalumu wa kukamata wahalifu wanaojihusisha na uvamizi ndani ya hifadhi hiyo ikiwemo vitendo vya ujangaili pamoja na ukataji wa miti, uchomaji wa mikaa,uwindaji haramu pamoja na uingzwaji wa mifugo ndani ya hifadhi hiyo na kusababisha uharibifu ndani ya hifadhi na kulaani pia hatua ya wananchi wa vijiji jirani kuingiza mifugo mara kwa mara ndani ya hifadhi jambo ambalo halikubakili kisheria na kimazingira.

Akizungumzia changamoto ya kudhibiti vitendo vya uharibifu wa mazingira vinavyofanywa na wavamizi wasiojali umuhimu wa uhifadhi meneja wa hifadhi ya msitu wa KISAMPA Bw.Ana bolli Amir amesema ukosefu wa walinzi wa kutosha pamoja na ukubwa wa eneo la msitu kumesababisha wao kupata wakati mgumu kulinda hifadhi hiyo ambayo pia rasimlimali wanyama wa hifadhi ambao wamekuwa wakiishi katika hifadhi hiyo kwa muda mrefu sasa.Katika opereshini hiyo ilifanikiwa kukamata magunia mbalimbali ya mkaa,ng”ombe na vipisi vya mbao huku wahusika wenye mizigo hiyo wakikimbia kusikojulikana na kumfanyikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja ambale alikiri kosa la kuharibu mazingida ndani ya hifadhi hiyo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment