Image
Image

Nicki Minaj amnasa Mmachinga akiuza T- Shirt zake bila kibali.


Pengine swala la kuibwa kwa kazi za wasanii mfano CD na T-Shirt fake zilizojaa kariakoo zikiuzwa na Wamachinga halipo tu nyumbani Bongo, au barani Afrika pekee bali ni mpaka nchi zilizoendelea.
Katika pitapita zake kwenye mitaa nchini Marekani female rapa Nicki Minaj aliweza kumbamba muuza nguo mtaani akiuuza T-Shirt ya albamu yake kwenye barabarani bila ruhusa kutoka kwa Nicki Minaj.
Nicki Minaj alikuwa anapita barabarani akiwa kwenye gari na bahati nzuri alimuona mfanya biashara huyo wa barabarani akiuza T- Shirt yenye ujumbe wa kupromote albamu yake mpya ya The Pink Print.
Nick aliamuakumfuata na kwenda kuuliza bei ya T- Shirt kabla ya kijana huyo kujibu alishtukia kama aliyeuliza swali hilo ni mwenye mali “Nicki Minaj” na kwakuwa bidhaa hiyo ilikuwa ni ya wizi kijana huyo aliamua kukimbia kwa kuvuka barabara upande wa pili.
Haikuwa rahisi kwa Nicki Kumkamata mwizi wake, kwani alikuwa yupo ndani ya gari.Watu na wasafiri waliokuwa katika eneo hilo walipiga yowe kwa kitendo cha Nicki kumshtukia muuza nguo huyo.
Naye kijana huyo alipofanikiwa kuvuka barabara alianza kumrekodi na kuanza kumpiga picha Nicki huku wapita njia wakizidi kupiga kelele za shangwe kwa kitendo cha Nicki kutupiana maneno na kijana huyo.
Nicki Minaj alitupia kipande cha video kwenye akaunt yake ya instagrama kuonyesha tukio hilo.

 

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment