Image
Image

Shambulizi la bomu katika msikiti mmoja Kusini mwa Saudi Arabia lateka maisha ya watu 13.


Wizara ya mambo ya ndani ya Saudi Arabia ilifahamisha kuwa kwa uchache watu 13 walifariki katika shambulizi la bomu lililotekelezwa katika msikiti mmoja ulioko katika mji wa Abha ulioko Kusini mwa nchi hiyo. Ujumbe uliotolewa na msemaji wa wizara hiyo ulisema kuwa watu wengine 9 walikuwa wamejeruhiwa huku 3 wakiwa wamejeruhiwa vibaya.
Msikiti ulioshambuliwa ulikuwa ukitumiwa na maafisa wa polisi wa kitengo cha SWAT. Kati ya waliouawa, 10 walikuwa maafisa wa polisi wa kitengo hicho huku 3 wakiwa ni wafanyikazi katika msikiti huo.
Ingawa taarifa yeyote kuhusu watekelezaji wa shambulio hilo haikutolewa, shambulio hilo linasemekana kuwa la kujitoa mhanga kwa kuwa mavazi yanayotumiwa na washambuliaji wa kujitoa mhanga yalipatikana katika eneo la tukio hilo.
Hili ndilo shambulizi kubwa zaidi kutekelezwa dhidi ya walinda usalama wa Saudi Arabia katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita. Wanajeshi na maafisa wa polisi nchini Saudi Arabia wamekuwa wakilengwa katika mashambulizi mbalimbali yanayotekelezwa na kundi la ISIS.
Kufikia sasa hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment