Watu 17 wakiwemo wanajeshi 12 wameripotiwa kupoteza maisha baada ya helikopta moja ya kijeshi kuanguka katika mji wa Zabul ulioko kusini mwa Afghanistan.
Afisa mkuu wa jeshi Ahmed Pamir, alitoa maelezo kwa waandishi wa habari na kuarifu kuanguka kwa helikopta hiyo hapo jana nyakati za mchana.
Akibainisha kuanguka kwa helikopta hiyo kutokana na matatizo ya kiufundi, Pamir alisema kuwa wametuma timu ya waokoaji kwenye eneo la ajali.
Wizara ya Ulinzi ya Afghanistan ilithibitisha kutokea kwa ajali hiyo ingawa haikutoa maelezo zaidi.
Wakati huo huo, msemaji wa kundi la Taliban alitangaza kuwa helikopta hiyo ililipuliwa kwa roketi na kudai kwamba wanajeshi 25 wa Afghanistan walifariki baada ya kuanguka.
0 comments:
Post a Comment