UNSMIL yatangaza tarehe ya kuanzishwa tena upya kwa mazungumzo kati ya makundi pinzani ya Libya.
Shirika la UN la UNSMIL limetangaza tarehe ya kuanzishwa tena upya kwa mazungumzo kati ya makundi pinzani yaliyoko nchini Libya.
Mazungumzo hayo yanatarajiwa kuanza nchini Morocco, siku ya Jumatatu tarehe 10 mwezi Agosti.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa mtandaoni kupitia tovuti rasmi ya UNSMIL, mjumbe maalum wa UN nchini Libya Bernardino Leon alitoa wito wa mazungumzo kwa lengo la kutatua mizozo baada ya kukutana na makundi yote pinzani.
Katika maelezo hayo yaliyotolewa Leon alisema, ‘‘Mazungumzo ya kutatua mizozo yanaungwa mkono na jumuiya ya kimataifa, na makundi yatakayokwenda kinyume yatakumbwa na vikwazo.’’
Maelezo zaidi yanaarifu kwamba makundi yote pinzani yamesikiliza wito wa Leon na kukubali kuanzisha mchakato wa mazungumzo ya maelewano siku ya Jumatatu nchini Morocco.
0 comments:
Post a Comment