Rais wa Senegal akemea na kulaani vikali shambulizi la kujitoa mhanga lililotekelezwa kwenye msikiti mmoja nchini Saudi Arabia.
Rais wa Senegal Macky Sall, amekemea na kulaani vikali shambulizi la kujitoa mhanga lililotekelezwa kwenye msikiti mmoja na kusababisha vifo vya watu 15 nchini Saudi Arabia.
Sall alimtumia Mfalme wa Saudi Arabia Salman bin Abdulaziz Al-Suud salamu za rambirambi, na kutoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu na jamaa katika shambulizi hilo.
Shambulizi hilo la kujito mhanga lilitekelezwa wakati wa swala ya adhuhuri kwenye msikiti mmoja uliokuwa ukitumiwa na maafisa wa usalama wa kitengo maalum katika mji wa Abha nchini Saudi Arabia.
Watu 15 wakiwemo maafisa 10 wa usalama walipoteza maisha kwenye shambulizi hilo.
0 comments:
Post a Comment